MAISHA YA MSANII WA MUZIKI SUPRIZE BABY
HAYA NDIO MAISHA HALISI YA MSANII WA MUZIKI SUPRIZE BABY
Msanii Nicholaus Baltazar(SUPRIZE BABY) Amezaliwa 10/9/1996 mini Arusha katika hospitali ya MountMeru hapo hapo mini Arusha.
Suprize baby Alisoma Elimu ya Awali na Kuendelea na Elimu ya Msingi Shule ya Msingi Daraja Mbili mini Arusha.
Mnamo mwaka 2000 Suprize alianza Masomo ya Awali ilipo fika mwaka 2003 Suprize aliendelea na masomo ya Msingi katika Shule ya Msingi daraja mbili ,Suprize alirudia tena darasa la pili katika Shule ya Msingi Sanawari ya juu iliyopo hapo hapo mkoani Arusha baada ya migogoro ya kifamilia aliondoka na Mamayake na kuamia Sanawari ya juu.Baada tena ya mama na baba take kurudiana Suprize alirudia tena darasa la pili katika shule ya Msingi darajambili hapo hapo mini Arusha.
SUPRIZE ALIPOANZA MUZIKI NA KUKIONA KIPAJI ALICHONACHO
Ilipofika mwaka 2008 Suprize alikuwa darasala tano,Kwa Mara nyingine baba na Mamayake tena waliachana,Suprize Aliishi na Mamayake mtaa wa Sinoni Ungalimited Arusha .hiki kipindi nilikuwa kigumu kwa Suprize na Mamayake kwani hapo ndipo walikula kwa tabu na kulala kwa tabu ,,huu wakati mgumu mama yake Suprize Alikitambua kipaji cha mwanae alipomuona na dalili za kuwa Msanii.ila livha ya mama take kujua kipaji cha mwanae alikichukulia juujuu kwa kisingizo ni Muhuni lakini Suprize hakusikiliza maneno wala hakukata tamaa alimwambia mama yake anandoto za kuwa kama Diamond Platinumz
SUPRIZE KUTAMBULIKA NA WATANZANIA KIMUZIKI
Mwaka 2010 Suprize Alimaliza darasa la Saba Akafanikiwa kuendelea na masomo ya secondary katika Shule ya Secondary Felix mrema iliyopo hapohapoa mini Arusha .
Suprize kulingana na hali walioishi na Mamayake kihasi hata cha kulala kwa bibi yake na kula Ugali ambao bado ni uji na mboga ukiwa chumvi..Mamayake alijitahidi akapangisha .Suprize alijitahifi sana kusoma lakini kwa mawazo ya kifamilia akiyafikiria yalimfanya Shuleni Ashuke wastani tofauti na ule wa kwake wa mwanzo.
Kipindi hichi Suprize alikuwa anajua kuandika mashairi yake binafsi na kujiimbia Akiwa mwenyewe.Mwaka 2014 Suprize alifanikiwa kumaliza masomo ya kidato cha NNE lakini kwa bahati mbaya hakuchaguliwa kuendelea na masomo hapo ndio Alipoanza kufanya kazi ndogondogo ili kuweza kula na kuvaaa yeye na mama yake .
Kabla Suprize ajamaliza kidato cha NNE wakati akiwa kidato cha Tatu aliweka Storia Shule ya Secondarily Felix Mrema na kuwekwa picha take kwenye Ubao wa Matangazo kwa ukumbusho kwa kufahamika kwa jina la Diamond Mdogo kwa kuweza kufanya kitu kikubwa na walimu hawakutegemea kwa Alichofanya Suprize ,Baada ya kwenda kwenye mashindano ya health club aliimba na kuja na cheti shule cha uimbaji bora wa shule za Arusha zote Alishika nafasi ya kwanza na kuipa jina Shule ya Sekondariy Felix mrema na alipofika shuleni alizawadiwa na mkuu wa shule Redio yenye thamani ya 120,000 baada ya kushinda na kuju na kombe shule kwenye mashindano ya Usalama barabarani(maamuzi yako barabarani ni hatima yetu fikiri kwanza) baada ya kuimba ndio Shule ya Secondary Felix mrema ikazidi kupata jina kupitia Suprize ,Suprize alishiriki kwenye mahafali mbalimbali ya Shule na kuimba alipendwa sana na kubatizwa jina Diamond mdogo .
SUPRIZE KUANZA MUZIKI RASMI.
Suprize baada ya kumaliza kidato cha NNE alianza muziki rasmi na kuacha kufanya mambo mengine na kuegemea kwenye kipaji chake akijua IPO siku atafaniniwa na kujulikana na watu Suprize hakukata tamaa alijichanga pesa aliyokuwa anaihifadhi ili aende studio.Suprize alipata studio ya kurecodia iliyofahamika kwa jina la LUCKY RECORDS.Suprize alianza kurecord remix za diamond kama UKIMWONA na UTANIPENDA Yeye aliimba NIKIPONA na UTANITOA zilivutia watu kusikiliza na kumpa moyo Suprize asikate tamaaa,,,,
Suprize baada ya kufanya hizo nyimbo alijipanga na kufanya nyimbo nyingine ambazo zilimpa fursa ya kupanda kwenye majukwaa ya maukumbi mbali mbali yaliyopo mjini Arusha kama TRIPO A,GOLDEN ROSE nakadhalika,,,,
Nyimbo alizofanya Suprize ni kama UMENIACHA,AIYOYO,SORRY,NUMBER ONE na kadhalika
MALENGO YA SUPRIZE YALIKUWA WAPI?
Suprize alijitahidi kwenye mziki japo alionekana mdogo hakukata tamaaa alijitahidi kupambana na hali yake ,kitu ambacho Suprize anakikumbuka ni siku akiwa kwa mashindano ya BSS(BONGO STAR SEARCH) ARUSHA ,alikatishwa tamaa na MASTER J Kwa kuambiwa rudi ukishabaleehe ila hakukata tamaa alijitahidi akashiriki mashindano ya SUPER NYOTA ARUSHA, na kufanikiwa kushika nafasi ya Tatu katika mkoa wa Arusha na kupewa fursa na zawadi na kupangwa kuiwakilisha Arusha kwa kupanda stage ya FIESTA Arusha na kufanya vizuri kwa kupokelewa na watu hapo ndio alipopata mashabiki na kumshukuru mwenyezi mungu.
MPAKA SASA SUPRIZE AJAPATA MENEGMENT!!
Kweli unaambiwa usikate tamaa ipo siku yako ni kweli hii ni kwawale wenye moyo wa kufika .Suprize mbali na yote aliyofanya Arusha hajafannikiwa mpaka sasa kupata MENEGMENT ila alichosema Suprize hatakata tamaa ya kuuacha muziki kwani ndo kipaji chake mpaka Leo hajafanikiwa kupata Meneger ila ajakata tamaa atafanya mziki na kufurahia kipaji chake na hataacha muziki mpaka siku aingie kaburini.Alisema Suprize anapigwa vita na babayake kwani wanafikiri muziki ni uhuni anavunywa moyo na wazazi na sio watu baki wakimwambia muziki hauwez kumtoa mpaka sasa hawaoni maendeleo lakini Suprize anasema yeyekwake anaona maendeleo kwani maendeleo sio kujenga Bali ni kuishi maisha ya AMANI nia furaha muda wote hayo ndio maendeleo aliyasema hayo Suprize baby mwanamuziki anayeiwakilisha ARUSHA vyema,,,
SIO KWA SIKIO TU BALI HATA KWA TASWIRA WAMJUA SUPRIZE BABY
Ni Swali je wajua utafika na wewe msomaji wa historia halisi ya Suprize baby Msanii mwanamuziki anayeiwakilisha ARUSHA vyema kwa wakati huu japo mpaka sasa hajapata Meneger ya kuisaport kazi Yake ya muziki ,,,,,Suprize alijipanga na kufanya video kwa Mara ya kwanza alifanya vizuri sana japo Ulikuwa ni marayakwanza kusimama na kamera alifanya vizur sana hiyo ilichangia hadi MCTV ARUSHA. wamfayie Interview bure kwasababu ya kujituma kwake ,,,
Nyimbo ambayo alifanya ni nyimbo yake iliyovutia watu wazima na watoto na vijana wa Marne hizi nyimbo hiyo ilifahamika kwa jina la SORRY unaweza kuitizama sasa"""""
Baada ya Sorry Suprize alipata collaboration na Msanii wa kenya aliyefahamika kwa jina la Samirr hapo ndipo ilimpa umaarufu kidogo wa kujulikana na nchini kenya kwani Samirr ulikuwa ni Msanii anayefahamika sana kenya na nimsanii Upcoming aliyechukua tuzo za Upcoming Artist Award nchini kenya na kupata umaarufu ,,,,,alifanikiwa kukutana na Suprize kwa studio za LUCKY RECORDS ARUSHA na kufanya collaboration ya nyimbo inayosumbua redio za kenyaikiwemo CTIZENI KENYA REDIO ,,nyimbo iliyokwenda kwa jina la DADAZETU ,,,,,
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni